Hapo zamani za kale kulikuwa na mfalme. Katika kijiji cha mfalme kulikuwa na mtu na mkewe ambao walipendana sana. Siku moja mtu huyu alienda safari.
Baada ya mtu
huyu kuondoka, mfalme alianza kufanya ziara katika kijiji chake. Alipokuwa
akipitia karibu na nyumba ya mtu huyo aliona bibi ya mtu huyo na akapendezwa sana na sura yake.
Aliporudi kwake
nyumbani alituma mtumishi wake aende akamwambie bibi huyo kuwa anampenda sana na angeenda
kumtembelea.
Bibi huyo
alirudisha ujumbe kwamba yeye alikuwa na bwanake ambae alimpenda sana.
Hata baada ya
kupewa ujumbe huo mfalme huyo hakukata tamaa. Alituma mtumishi wake arudi
akamwambie yule bibi kuwa angeenda kumtembelea.
Alipoenda
kumtembelea huyo bibi kulikuwa usiku. Mfa;me alikuta bibi huyo tayari.
Alikaribishwa vyema na akaandaliwa chakula. Chakula alichoandaliwa kilikuwa na
rangi tatu tofauti. Baada ya kumaliza chakula hicho, bibi huyo alimuuliza
mfalme
Chakula hicho
kilikuwaje?
Mfalme akajibu,
“Hata ingawa
chakula
hicho kilikuwa
na rangi
tatu tofauti,
ladha yake
ilikuwa moja.”
Bibi huyo
akajibu
“Vivyo hivyo
ndivyo
wanawake
walivyo.
wana sura
mbalimbali
lakini ladha yao ni moja.”
Bibi huyo
aliendelea kumwambia mfalme kuwa atulie na aache kumsumbua kwa vile yeye
alikuwa na bwanake.
Mfalme akaona
aibu na akatoka mbio na katika mbio hizi akaacha kiatu chake.
Mume wa bibi
huyo aliporudi alikuta kiatu cha mfalme kwake na akashangaa sana.
Alijiuliza
“Mfalme
alikujaje kwangu?”
Aliamua kuwa ni
lazima pawe na uhusiano kati ya mkewe na mfalme. Aliamua kumwacha mkewe.
Mkewe alipoona
kuwa mumewe hakuwa na haja naye, alienda kumshitaki kwa mfalme. alimsimulia
kisa cha mtu ambaye alikuwa na shamba. Alikuwa anapalilia shamba lake kwa juhudi na uangalifu wa hali ya juu.
Shamba hilo lilikuwa na matunda,
waua, miti na
kila kitu. Watu
walikutwa
wanapendezwa na shamba hilo
lakini sasa mtu
huyo amelitupa shamba hilo
lake. Halijali
tena. Halimi na matunda
na mazao mengine
hayapatikani tena.
Mfalme alielewa
ujumbe uliokusudiwa na huyo bibi
kutokana na kisa
hicho. Aliita mtumishi wake
na akamtuma
akamwite bwana wa bibi huyo.
Bwana wa bibi
huyo aliitika wito wa mfalme
na akaenda.
Alipofika huko, alipewa mashtaka
ambayo yalikuwa
yametolewa na mkewe.
Aliyakubali
lakini akajitetea. Alisema kuwa alitupa shamba lake tu
baada ya kuona wayo la shamba ambaye alikuwa akupitia shambani mwake. Aliona ni
hatari kuendelea kulima shamba hilo
na akaogoppa na akamua kuliacha asije akahatarisha maisha yake.
Mfalme alielewa
utetezi wa bwana huyo ……. Alimweleza kuwa ni kweli kuwa simba alikuwa amepitia
shambani mwake lakini hakugusa chochote. Kwa hivyo mfalme alimuhimiza yule
bwana arudi akapalilie shamba lake
kama alivyokuwa akifanya
hapo awali.
(Jibu maswali
yafuatayokutokana na hadithi hii)
(1) Eleza
maudhui muhimu ambayo yanajitokeza katika hadithi hii
(2) Bainisha
dhamira kuu na dhamira ndogo amazo zinapatikana katika hadithi hii.
(3) Msanii
ametumia mbinu zipi katika kuwasilisha maudhui yake?
Katika hadithi
hii ujumbe tunaoupata ni kwamba ugomvi waweza kutokea kwa sababu ya mambo
yasiyo na msingi. Kwa mfano tunaonyeshwa jinsi mfalme alivyoelimishwa kuhusu
uchu wake na kuonyeshwa kwa fumbo la chakula kuwa hata ingawa wanawake
hujitokeza kwa sura mbalimbali wote ni kitu kimoja na ladha zao ni sawa.
Vile vile
tunaonyeshwa jinsi ugomvi unavyoweza kuzuka baina ya mtu na mkewekwa sababu ya
ukosefu wa mawasiliano. Kama kungekuwa na
uelewano bibi angalimueleza mumewe kuhusu safari ya mfalme nyumbani jwao na
yale yaliyotendeka. Mawasiliano hayo yangezuia mashtaka waliopeleka kwa mfalme
ambaye ndiye alikuwa chanzo cha mgogoro wao.