Pamoja Tunaweza Saccos (PT-SACCOS) ni kikundi cha ushirika kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya utoaji wa huduma za kifedha kwa wanachama wake  kwa mtindo wa kukopa na kuweka. PT-SACCOS inafanya shughuli zake katika eneo la Makumbusho –DSM.
MAJUKUMU YA NAFASI HUSIKA
Kuandaa fomu za maombi ya mikopo
Kupokea marejesho na michango ya wanachama
Kupeleka cheki benki
Kuwa kiungo kati ya PT-SACCOS na ofisi ya ushirika ya Wilaya/Mkoa
Kuandaa na kutunza vitabu vya mahesabu.
Na kazi nyingine utakazopangiwa na uongozi
NB: Uendeshaji wa shughuli za PTSACCOS hazihitaji kukaa ofisini muda wote, utafanya pale utakapohitajika.
MAELEZO KWA MWOMBAJI:
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe Mtanzania mwenye umri kuanzia 20-30
Awe na Elimu ya Uhasibu/Utunzaji wa vitabu vya fedha kwa ngazi ya cheti au stashahada na aliyefaulu vema masomo ya hisabati na kiingereza kwa kidato cha nne/sita.
Mweny elimu ya Ushirika kutoka Chuo kikuu cha Ushirika moshi atapewa kipaumbele
Awe mchapa kazi na mwenye kujituma na kujifuza kwa haraka.
Awe na uzoefu wa kuandaa taarifa za fedha katika taasisi za fedha au vyama vya ushirika  
Awe na ujuzi wa kutumia vizuri kompyuta
Mshahara ni maelewano

Maombi yote yaandikwe kwa mkono na yatumwe ikiwa ni pamoja na wasifu binafsi (CV) na vivuli vya vyeti ( Cheti cha kuzaliwa na Vyeti vya taaluma)
Yatumwe kwa:

Mwenyekiti,
PT SACCOS
DSM
Kupitia baua pepe   ptsaccos2011@gmail.com    na/au     dsbonde@yahoo.com
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25 Sep 2016

NB: Wenye elimu zaidi ya ngazi ya stashahada wasiombe.